Tunda Athibitisha kumwagana na Young D

Muuza nyago macha-chari Bongo, Tunda Sebastian amefunguka kumwagana na mwandani wake wa muda mrefu, ambaye ni staa wa Bongo Fleva, David Genzi ‘Young D’ na kusema ameamua kujiweka kando kwenye maswala ya mapenzi.

Akipiga stori na chanzo cha uhakika baada ya kumbananisha kuhusiana na tetesi za uhusiano wake kuvunjika kutokana Young D kubaini anatoka na mwanamuziki mwenzake (jina kapuni) ndipo akaeleza kuwa, ishu hiyo haina ukweli ila ameachana na mwandani wake huyo kwa sababu ambazo hawezi kuzianika kwa sasa.

“Hayo ya kutoka na huyo msanii si kweli na kuhusu Young D nimeshaachana, sifikirii kuwa na msanii yeyote na sihitaji mpenzi kwa sasa,” alisema.
Previous
Next Post »

Total Pageviews