Kwa kava hili wimbo ujao wa Gigi Money ‘Tikisa Supu’ utakutana na yaliyomkuta ‘Chura’ wa Snura

 
Mabinti wamekata ringi na hawataki kusikia kitu kinaitwa Maadili ya Mtanzania.Inaitwa kujilipua just to get that money no matter what! 

Video vixen anayejaribu bahati yake kwenye muziki, Gigi Money alisema wazi kuwa wimbo wake ujao 'Tikisa Supu' ni wa kuweka mbali na watoto na kwa kava la single hiyo sasa tumepata jibu la kwanini alituonya mapema. 

Msichana huyo amepost kwenye Instagram picha ya kava la wimbo huo aliomshirikisha Matonya ikimuonesha akiwa amevaa vazi maalum la wapishi lililomfunika kifuani tu na huku akiwa amevaa thong (nguo ya ndani iliyoshikiliwa na mikanda tu) na hivyo kimsingi ni kama yupo mtupu.

Picha hiyo tayari imesababisha mjadala mtandaoni huku wengine wakishindwa kuvumilia na kumwogesha Gigy mvua ya matusi. Kuna kila dalili kuwa wimbo huo unaweza kukutana na adhabu ile ile iliyopewa Chura ya Snura na wizara husika.
Previous
Next Post »

Total Pageviews