Machangudoa Waja Juu Wataka Biashara yao Itambulike



Baadhi ya wanawake wanaojiuza katika mitaa ya Majengo B na Fisi, mjini Mpanda mkoani Katavi wameitaka Serikali kuandaa utaratibu wa kuwatambua ili nao waweze kulipa kodi na kuliingizia taifa pato kutokana na shughuli wanayofanya ya kuuza miili yao.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana usiku, baadhi yawanawake hao walisema wanafanya kazi kama zilivyo kazi nyingine kwani zinawaingizia kipato kizuri kinachowasaidia kutimiza mahitaji yao ya msingi hivyo kazi hiyo inapaswa kuheshimiwa na kutambuliwa na serikali.


Mmoja wa wanawake hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Joyce, alisema ni wazi Serikali ikiandaa utaratibu mzuri wa kuwatambua itawafanya waweze kulipa kodi ambayo italiongezea pato taifa tofauti na ilivyo sasa ambapo wamekuwa hawalipi kodi kwa kuwa hawatambuliwi.


" Sisi kazi yetu ina kipato kizuri kutokana na makubaliano yanayofanyika kati na wateja wetu lakini Serikali haitaki kututambua hivyo sio rahisi hata kututaka tulipe kodi, nchi nyingine watu kama sisi tumetambuliwa na tunalipa kodi serikalini" alisema Rosemary Kazeze.


Aliongeza kwamba kipindi hiki ambacho Serikali inatafakari au haioni umuhimu wa wao kutolipa kodi, anawashauri kina dada poa wenzake kuacha tabia ya kukwepa kwenda Nyumba za kulala wageni zinazotambuliwa na Serikali kwani kufanya  hivyo kunaikosesha serikali mapato


Alisema kuwa siku za nyuma walikuwa wanafanya biashara hiyo katika madanguro kitendo ambacho polisi walikuwa wakiwasumbua kwa kuwakamata kutokana na misako ya mara kwa mara, lakini hivi sasa hawasumbuliwi kwani wamepanga vyumba katika gesti halali na wanalipia vyumba hivyo na mmiliki analipa kodi kwa msingi huo nao wanachangia pato la taifa.


“ Kaka yangu mwandishi tunashukuru sana hata wewe kutufikia, wanatudharau na kutunyanyasa sisi lakini wateja wetu wakubwa ni hao hao viongozi wa serikali na tasisi nyingine lakini wajue kufanya biashara ya ukahaba sio sababu ya kuto muunga mkono Rais wetu katika suala la mapato ya serikali”…alisema Mayasa Hussein
Previous
Next Post »

Total Pageviews