Shilole aonyesha hii video akiwa na Vanessa Mdee saloon ambapo ugomvi wao ndipo ulianzia!


Yadaiwa kuwa Vanessa Mdee na Shilole walikuwa pamoja kwenye saloon ya American nails ambapo wawili hao walikuwa pamoja kwaajili ya kurembwa kama ilivyo kawaida ya wanawake.

Lakini udaku unasema kuwa mtu wa karibu na Shilole alibaki hapo saloon ambapo Vanessa Mdee baada yakuona Shilole kaondoka aliongea maneno yasiokuwa mazuri kwa Shilole na kwasiri alirekodiwa na kumtumia Shilole.

Bado haijajulikana wazi kuwa nimaneno gani hayo lakini inadaiwa kuwa nikuhusiana na ngoma ya Say My Name yakwake Shilole aliyo msirikisha mtunzi wa ngoma hiyo Barnaba.

Jana Vanessa Mdee amehojiwa kwenye kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio na kusema hayupo tayari kuzungumzia lolote kuhusiana na ugomvi huo.


Previous
Next Post »

Total Pageviews