Rama Dee afungukia juu ya penzi lake la dhati kwa Lady Jaydee

Nguli na mkongwe wa muziki wa R&B nchini Rama Dee ametoa sababu ya kuonesha ushirikiano mkubwa katika harakati za muimbaji Lady Laydee.

Akizungumza na mtangazaji wa kipindi cha Ladha 3600 cha EFM, Jabir Saleh, Rama Dee alisema anaendelea kumsupport Jide sababu ni msanii anayepambana na yupo serious kuhakikisha anafanya kilicho bora zaidi ili kuilinda heshima yake katika muziki.

Rama aliongeza kuwa Jide ameweka historia kubwa sana katika tamasha la Naamka Tena Concert lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City kwani ni mfano tosha kwa wasanii wengine ambao hawapo serious na game.

Hitmaker huyo wa Kipenda Roho kwa sasa yupo nyumbani na ametoa shukrani kwa mashabiki wake na kuwaahidi kuwa atawapa surprise kabla hajaondoka kurudi Australia ambako ndiko makazi yake yaliko kwa sasa.

Muimbaji huyo amemuoa raia wa nchini Australia na wana watoto wawili pamoja.
Previous
Next Post »

Total Pageviews