Diva asema anataka kuzaa mtoto moja tu kisha afunge kizazi baada ya hapo


Star wa Clouds FM, Diva, amefunguka na amesema kwenye maisha yake anataka azae Mtoto Mmoja tu wa Kiume na kufunga Kizazi baada ya hapo.

Akiongea na Makorokocho, Diva amesema amekuwa akisumbuliwa na Maumivu ya Tumbo toka anakuwa binti na imefikia kipindi analazwa kwa siku 1 au 2 toka anasoma ili apate matibabu akiwa karibu na madaktari sababu wakati anasoma alikuwa anafika stage anazimia maumivu hayo yakizidi lakini baada ya kuwa mkubwa yakaanza kupungua.

Mwaka jana, 2015, Diva alifanyiwa operesheni katika hospital ya Sanitas na ushauri alioambiwa ni akae kidogo halafu azae. Na sasa star uyo amefunguka na kusema atazaa Mtoto Mmoja tu na anaombea awe wa Kiume na baada ya hapo atafunga kizazi.

"Naogopa sana kubeba mimba na kuzaa, so wil do that Mara Moja tu Kwa Miezi 9 then after that Ntafunga kizazi na Mtoto wangu nitaenda jifungulia nchi za Marekani ili apate uraia wa huko" Alisema Diva.
Previous
Next Post »

Total Pageviews