Giggy Money asema anapenda penzi la mpenzi wake mpya 'Matonya' kwakuwa anajua sana kuhonga


Mwanadada chakaramu mitandaoni na mwanamuziki Giggy Money, amesema anampenda sana mpenzi wake wa sasa ambae pia ni msanii wa Bongo flava Seif ‘Matonya’ Shaaban kwa kuwa ni muhongaji mzuri.

Akizungumza kupitia kipindi cha Kubamba cha Times Fm juzi Jumapili, Giggy ameweka wazi mahusiano yake na Matonya ambapo alimpigia simu ‘live’ radioni na kuzungumza kimahaba huku akijinasibu kwa dhati kuwa Matonya ni miongoni mwa Wapenzi wanaohonga vizuri Zaidi. “Nimechoka kuulizwa kila siku juu ya Matonya ngoja nimpigie umsikie mwenyewe(anampigia)” Alisema Giggy na kumpigia simu Matonya. “Unajua nampenda sana Tonya Coz anajua kuhonga aisee, namuelewa sana yani” Alimaliza.
Previous
Next Post »

Total Pageviews